Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula anatoa pole kwa Azam TV, Familia,s Ndugu, Jamaa na Marafiki kufuatia kifo Cha waandishi wa habari watano wa kituo hicho waliokuwa wakisafiri kikazi kutoka mkoa wa Dar es Salaam kuelekea mkoa wa Geita.
Aidha Mhe Mabula anawataka kuwa watulivu na kuungana pamoja kuwaombea majeruhi wote ili wapone haraka na kuendelea na ujenzi wa taifa.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela


No comments:
Post a Comment