Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mwanza Mhe Kemilembe Lwota amekabidhi Vitanda na Mashuka katika hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza ikiwa ni jitihda zake binafsi katika kuhakikisha anaungana na Serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Akiwa hospitali ya wilaya ya Misungwi, Mhe Kemilembe Lwota amesema kuwa anatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli katika kuhakikisha inaboresha huduma za afya hasa za mama na mtoto, Huku akiwahimiza wananchi kuwa ni wajibu wa kila mmoja na jamii kwa ujumla kuunga mkono jitihada hizo
‘.. Kila mmoja kwa nafasi yake anaowajibu wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya, Ndio maana mie leo kwa nafasi yangu nmeamua kutoa msaada huu wa vitanda kumi, magodoro kumi na mashuka thelathini ili kuunga mkono jitihada hizi za Serikali ..’ Alisema
Aidha Mhe Kemilembe katika kuhakikisha anawakomboa wanawake wa wilaya hiyo kiuchumi na kuunga mkono ujenzi wa Tanzania ya Viwanda amewaahidi kuanzisha mradi wa kiwanda kidogo kwa kuanza na kuwapa vyerehani 5 watakavyokuwa wanavitumia kuzalisha bidhaa mbalimbali kulingana na uhitaji wa soko.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Mhe Antony Bahebe amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada wa Vitanda na mashuka katika hospitali anayoisimamia huku akimtaka mganga mkuu wa wilaya hiyo Dkt Zabron Masatu kuvitunza vifaa hivyo sambamba na kuwapongeza kina mama wa mkoa wa Mwanza kwa kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua mbunge huyo anaejali shida za wananchi.
Katika hatua nyengine Mhe Kemilembe Lwota ameitembea shule ya wanafunzi wenye uhitaji maalum ya Mitindo inayofundisha wanafunzi Viziwi, Vipofu na wenye ulemavu ambapo amegawa mashuka shuleni hapo, amegawa vinywaji, na fedha taslimu kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofanyika mkoani Mtwara mapema mwaka huu.

















No comments:
Post a Comment