Thursday, August 1, 2019

DKT ANGELINE MABULA: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KUFIKIA NCHI YA VIWANDA

Sekta binafsi inayo mchango mkubwa katika kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Magufuli ya kuwa na nchi yenye uchumi wa kati kupitia Viwanda 


Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae  pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akifunga maonesho ya siku 3 kuanzia Julai 29-31, 2019 ya kitaaluma yaliyokuwa yakiendeshwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mtakatifu Joseph katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza ambapo amesema kuwa sekta binafsi inao mchango mkubwa wa kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuzalisha wataalamu na kubuni mbinu mbadala za kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii 


‘.. Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi katika kufikia Tanzania ya viwanda, Na niwatie moyo kuendelea na kazi hii  kwa mara nyengine ..’  Alisema


Aidha amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo bila kujali dini zao, kabila, rangi au mahali wanapotoka huku akiomba kufanyika tena kwa maonesho hayo kwa mara nyengine mfululizo katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa mkoa huo wenye ari ya kujifunza masomo ya Sayansi waweze kupata fursa hiyo kiurahisi.


Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Mtakatifu Joseph, Profesa Eliab Opiyo mbali na kumshukuru Mhe Mabula kwa kukubali kufunga maonesho hayo,  kutoa ufadhili wa masomo wenye thamani ya zaidi ya bilioni moja na milioni mia nne kwa wanafunzi watakajiunga na chuo hicho kama ada ya asilimia tano itakayotakiwa kulipwa, ameongeza kuwa lengo la maonesho hayo ni kuonyesha ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Joseph  Tanzania  na kuhamasisha wanafunzi nchini kote kupenda masomo ya Sayansi kwa kushirikisha shule 18 za Sekondari  za mkoa wa Mwanza ikiwemo Bujingwa, Buswelu, Bwiru, Eden Valley, Holly family, Mbugani, Mirongo, Mwanza, Nganza, Nsumba, Nyakabungo, Nyamanoro, Ole Njolay, Pamba, Pasiansi, Mtakatifu Joseph na Thaqaafa.











No comments:

Post a Comment