Thursday, August 1, 2019

KATIBU MKUU CCM ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MBUNGE WA ILEMELA.

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Mhe Dkt Bashiru Ally Kakurwa ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi inayofanywa na mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula  kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Hayo ameyabainisha wakati wa mkutano mkuu wa jimbo la Ilemela wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi tangu Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli kuingia madarakani, Mkutano uliofanyika katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo katibu mkuu huyo  amesema kuwa anaridhishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na mbunge wa jimbo hilo katika kuwatumikia wananchi wake licha ya kuwa na majukumu mengine ya kitaifa kama Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

‘.. Mbunge wenu wa Jimbo la Ilemela anafanya kazi kubwa na si kwa Ilemela peke yake, Anafanya kazi kubwa hata katika sekta ya Ardhi yeye na Waziri wake, Kati ya Mawaziri na Manaibu Waziri tunaofanya mawasiliano ya karibu sana ni pamoja na mbunge wenu ..’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Bashiru amewataka wakuu wa mikoa wote nchini kuhakikisha wanasimamia vyema katazo la matumizi ya Lumbesa na kudhibiti vipimo vya kinyonyaji kwa wakulima wote hasa katika zao la Dengu.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja  wa Vijana ya Chama hicho (UVCCM ) Ndugu Kheri James amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na CCM huku akiwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono ili iendelee kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo huku moja ya mjumbe wa kamati kuu ya CCM Mhe Munde Tambwe wananchi waliohudhuria mkutano huo kuhakikisha wanaendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi na viongozi wake.

Katika mkutano huo mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amepata nafasi ya kueleza shughuli za maendeleo zilizotekelezwa katika jimbo lake kupitia Serikali kuu, Halmashauri, wadau wa maendeleo na ushirikiano wa wananchi katika sekta zote za kiuchumi, kijamii, michezo, siasa, miundombinu, elimu, afya, ardhi na mipango miji kwa wananchi wake huku Dkt Bashiru Ally akihitimisha kwa kutembelea eneo ilipojengwa ofisi ya CCM ya wilaya hiyo na kuahidi kutoa msaada kwaajili ya kuhakikisha inakamilika mapema kufikia Mei 05, 2019.

'Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'


Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
Julai 30, 2019.












No comments:

Post a Comment