Wednesday, August 14, 2019

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AUNGANA NA BODABODA WA TABORA KUNUSURU MAJERUHI AJALI YA MOTO MORO.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameungana na waendesha bodaboda wa manispaa ya Tabora kwaajili ya zoezi la kuchangia damu ili kunusuru hali za majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni mkoa wa Morogoro. 

Akizungumza  wakati wa zoezi hilo la kuchangia damu, Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka waTanzania kuungana na Rais Mhe Dkt John Magufuli katika kunusuru majeruhi wa ajali hiyo kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake na kujitoa kwa kile kinachowezekana ili kuhakikisha wahanga hao wanarejea katika hali zao za kawaida na kuendelea na ujenzi wa taifa

‘.. Niwaombe tumuunge mkono mheshimiwa Rais kwa kila mmoja wetu kujitoa kwa nafasi yake ili tunusuru wenzetu hawa waliopata ajali ya moto na kuwaombea kwa Mungu wale wenzetu wote waliotangulia mbele za haki ..’ Alisema

Aidha Mhe Mabula amewaasa waendeshaji wa vyombo vya moto kuwa makini na kufuata sheria na taratibu za barabarani ili kuepusha ajali zisizo na ulazima.

Katika hatua nyengine, Naibu Waziri huyo ameendelea na ziara ya kikazi mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Idara ya Ardhi na kusikiliza kero za ardhi kwa wananchi.





No comments:

Post a Comment