KATIBU wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kenani Kihongosi amesema katika uchaguzi mkuu
mwaka huu Chama hicho ndicho chenye Ilani bora kuliko kipindi chochote
kile kwani imebeba matumaini ya Watanzania nchini.
Akizungumza
leo Oktoba 27,2025 mbele ya Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) pamoja na
makundi mengine ya kijamii Kihongosi amesema matumani hayo ya Watanzania
yamebebwa kuanzia vijana, wanawake na makundi mbalimbali wakiwemo
kinababa, watoto na wazee wenye mahitaji maalum.
Amebainishq
kwamba Ilani ya CCM inaingia mpaka kwenye familia palipo na kitovu cha
ujenzi wa maadili ya taifa."Hivyo tunaona ni kwa namna gani Ilani ya
CCM imesheheni mambo mtambuka yanayokwenda kuleta majawabu ya
Watanzania.
“Ilani ya CCM inatoa mwanga wa ajira na ustawi wa
jamii. Inaleta suluhisho katika sekta ya afya.Inaahidi mapinduzi ya
kiuchumi na uzalishaji. Dk. Samia anataka kuijenga Tanzania ambayo
rasilimali zetu zinaongezwa thamani kuanzia ngazi ya wilaya na mikoa.
“Mgombea
wetu amekuwa akisema atakwenda kuanzisha kongani za viwanda kuanzia
kwenye wilaya, mikoa ili kuongeza thamani ya mazao ambayo yatakuwa
yanazalishwa katika mikoa na wilaya husika. Hii itakwenda kufungua fursa
kubwa kiuchumi."
“Anafanya hivyo kwa kuwa anajua hatua hizo
zitakwenda kumkomboa kiuchumi mwananchi kwa kumwezesha kuuza bidhaa
badala ya malighafi.Ilani ya CCM ni mwanzo na mwisho wa kero za maji kwa
kuwa serikali inakwenda kuanzia gridi ya maji ya taifa.
“Kuzalisha
umeme megawati 8,000 ambayo ni mara mbili zaidi ya umeme uliokuwepo
sasa. Katika sekta binafsi, Ilani inakwenda kupewa kipaumbele na nguvu
kuliko wakati wowote nchini kwani CCM inataka kuendea muhula kwa kuleta
tija katika kilimo kwa kulima na kufuga kisasa.
"Ndiyo maana kuna
programu za chanjo ambazo serikali inatoa kwa wafugaji kuhakikisha
mifugo nchi nzima inachanjwa ili wafugaji waweze kufuga kwa tija
utakaoakisi maendeleo ya sasa," amesema.
Akifafanua zaidi amesema
katika sekta ya madini CCM imeahidi kuikuza, huku pia ikiahidi
kuboresha makazi ya wananchi kwa kujenga miundombinu zaidi ili kila kona
ya nchi ifikike kwa urahisi.
"Kwa msisitizo Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi imegusa kila eneo na huo ndiyo mwelekeo wa CCM ndani ya taifa
hili," amesema Kihongosi wakati anazungumza na makundi hayo ikiwa
imebakia siku moja Wanzania kwenda kupiga kura katika Uchaguzi mkuu
unaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Monday, October 27, 2025
CCM INAJIVUNIA UBORA WA ILANI YA UCHAGUZI MKUU ILIYOBEBA MATUMAINI YA WATANZANIA WOTE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment