Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
nchini Bi. Bella Bird.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi.
Bella Bird ambaye alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu,
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia nchini Bi. Bella Bird mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini
kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha na Makamu wa Rais Makamu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo
amkutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
nchini Bi. Bella Bird, Ikulu jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais na
Mkurugenzi huyo walizungumzia masuala mbalimbali ya Lishe kwa akina Mama
na namna ukosefu wa lishe bora unavyopelekea vifo vya akina mama na
watoto wakati na baada ya kujifungua. Aidha wamesisitiza suala la Elimu
ya Lishe Bora kwa wakina mama hao ili kukabiliana na tatizo. Makamu wa
Rais aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuwasaidia wakina mama wa Kitanzania
na kuitaka iendelee kufanya hivyo hasa wakati huu ambapo nchi inaenda
kwenye uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment