Mbunge jimbo la Nyamagana aitaka MWAUWASA shirika la
Usambazaji Maji safi na salama mkoani Mwanza kutatua kero ya maji kata
ya Mandu ndani ya Siku saba.
Mhe Stanslaus Mabula amesema hayo katika ziara yake kukagua
miradi ya Maendeleo kata ya Mandu kujionea mradi wa usambazaji Maji
Mtaa Wa Kisiwani ambao utakuwa mkombozi katika Kata hiyo kwa wananchi
waishio maeneo hayo.
Sioni iko haja wananchi takribani 2000 kutaabika zaidi ya
wiki moja kwa ukosefu wa Maji safi kwa mradi ambao umekamilika kwa
asilimia 70%. Natambua usambazaji huu umekwenda mita za urefu 3070 na
ni mita za urefu 1050 zimebaki. Kwani Ilani ya Ilani ya uchaguzi ya CCM
2015-2020 imejiekeza kutatua kero ya Maji kwa lengo la kumtua kila
Mwanamke ndoo ya Maji kichwani. Alisema.
Imetolewa na:Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana
No comments:
Post a Comment