Mhe Stanslaus Mabula amebainisha hayo alipokuwa anakagua
uwanja Wa shule ya Shigunga iliyopo kata ya Mandu katika halmashauli ya
Jiji la Mwanza. Amesema Ofisi yake kwa kushirikiano na halmashauli
inakarabati uwanja Wa shule hiyo utakao ghalimu takribani shillingi
milioni moja na nusu fedha za Tanzania zinazotumika katika usawazishaji
wa uwanja, umwagaji wa mafuta, upakaji wa rangi pamoja na uwekaji wa
magoli mapya utakao kamilika ndani ya wiki mbili.
Nia yangu nikuona mchezo unakuwa ni ajira kwa wana
Nyamagana wenye vipaji, na nilazima tukubali kujenga msingi imara
inayokuza michezo mashuleni, nitalisimamia hili katika uongozi wangu.
Nimeanza na mpira wa mguu kisha vitafuata viwanja vya michezo ya kikapu
na Pete. Alisema.
Imetolewa na:-Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana
No comments:
Post a Comment