Monday, September 18, 2017

MWAKILISHI NA MBUNGE JIMBO LA TUNGUU WATOA FEDHA KWA VIKUNDI 13 VYA USHIRIKA SHEHIA ZA UNGUJA UKUU

 
Mwakilishi wa Jimbo Tunguu Zanzibar Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla ya kukabidhi fedha Vikundi 13 vya Ushirika vya Wananchi wa Kae Pwani Unguja. Mchango huo umetolewa na Mbunge na Mwakilishi kuchangia vikundi hivyo kwa ajili ya kutunisha mifuko ya vikundi vya vinavyojishughulisha na ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa na kilimo na kukupeshana, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Ungua Ukuu Kae Pwani.
 Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane, Hatutaki Shari, Nia Njema, Aso Mtu Ana Mungu, Siri Moyoni, Tuwe Nao, Pita na Zako, Hatutaki Kero, Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu, Hawavumi, Imani na Wajibu Wetu.
 
Baadhi wa Viongozi wa Vikundi vya Ushirika katika Shehia za Kae Pwani Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla hiyo. 
 

No comments:

Post a Comment