Mwandishi Yusuph Ludimo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ametembelea mradi wa
Ujenzi wa Vyoo kwa Shule ya Msingi Buzuruga, Shule ya Msingi Nyambiti na
Shule ya Msingi Isenga iliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali kuu
(Wizara ya Maji) ikishirikiana na Benki ya Dunia kupitia mradi wa
Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ya Ziwa Viktoria ( LVEMP )
Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Mhe Dkt
Angeline Mabula mbali na kushukuru kwa Ujenzi wa miradi ndani ya Jimbo
lake amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuitunza ili iwanufaishe
kwa muda mrefu huku akiomba kusaidiwa ujenzi wa Vyoo vipya na vya kisasa
katika maeneo ya Mialo ya Ziwa Viktoria inayopatikana Ilemela sambamba
na sehemu za kisasa za kukaushia Samaki pindi wanapovuliwa
‘… Tunawashukuru wenzetu wa LVEMP kwa mradi huu lakini pia
tumewaomba na watatusaidia, Lengo langu kubwa ni kule kwenye maeneo ya
mialo unajua kule nako kuna uhitaji mkubwa wa kuwa na vyoo, Lakini kuna
uhitaji mkubwa zaidi wa kuwa na maeneo ya kuwa wanaweza kukaushia samaki
wao vizuri katika vichanja vya kisasa ambavyo ni rafiki wa mazingira …’
Alisema
Kwa upande wake mratibu mradi huo waUtunzaji mazingira ya
Ziwa Viktoria LVEMP Ndugu Omary Mnyanza amefafanua juu ya lengo kuu la
mradi ambalo ni uhifadhi na utunzaji wa mazingira na kusaidia afya za
wananchi huku akimhakikishia Mhe mbunge wa Jimbo la Ilemela juu ya
utekelezaji wa ombi lake la ujenzi wa Vyoo vya Kisasa na Vichanja vya
kukaushia Samaki maeneo ya Mialo ya Ilemela na kuhitimisha kwa kuwataka
wananchi kuacha kujisaidia ovyo na kuchafua Ziwa Viktoria
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
02.01.2017






No comments:
Post a Comment