Serikali
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema wanafunzi
wanaosoma katika shule binafasi wataendelea kutozwa ada ya mitihani ya
taifa kwa kuwa programu ya elimu bila malipo haizihusu shule hizo hivyo
wazazi na walezi ni jukumu lao kugharamia huduma hizo.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mei 15, 2018 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, William Ole Nasha Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 29
mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati
akijibu la Mbunge Viti Maalum Ester Mahawe aliyetaka kujua ni lini
serikali itafuta ada ya mitihani ya Taifa kwa shule za msingi na
sekondari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule binafsi ?.
"Serikali
inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika utoaji elimu nchini. Ili
kuhakikisha mazingira rafiki katika utoaji wa elimu serikali imekuwa
ikifanya majadiliano na sekta binafsi kwa lengo la kuondoa changamoto
mbalimbali zinazowakabiri.
"Katika
utekelezaji wa mpango wa elimu bila ya malipo, serikali ilifuta ada na
michango ya lazima katika shule za umma ngazi ya elimu msingi hadi
kidato cha nne", amesema Olenasha
Pamoja
na hayo, Naibu Waziri Olenasha ameendelea kwa kusema "ada na michango
hiyo iliyokuwa inalipwa na wazazi au walezi kwasasa inagharamiwa na
serikali, mpango huu haujazihusisha shule binafsi pamoja na umma ngazi
ya kidato cha tano na sita. Hivyo shule hizo zitaendelea na utaratibu wa
wazazi au walezi kulipa ada za mitihani ya Taifa".
Kwa
upande mwingine, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William
Ole Nasha amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya utoaji
elimu nchini kadri uwezo wa kifedha utakaporuhusu kufanya hivyo.

No comments:
Post a Comment