Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuingia kwa ugonjwa wa Chikungunya
nchini baada ya watu wanne waliotokea nchini Kenya kubainika kuwa na
dalili zinazofanana na ugonjwa huo.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo jijini katika ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa Habari.
“Mnamo
tarehe 20, Mwezi Juni, 2018 wasafiri wanne wa familia moja waliotokea
tena Mombasa nchini Kenya walishukiwa kuwa na ugonjwa huu baada ya kuwa
na dalili zinazofanana na ugonjwa wa homa ya Chikungunya kwenye kutuo
cha mpakani cha Holili kilichopo wilayani Rombo mkoani Kiliamanjaro”,
alisema Mhe. Ummy
Waziri
Ummy aliwatoa hofu wananchi kuwa Ugonjwa huu si mpya katika nchi yetu
kwani hapa nchini uligundulika katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania,
sehemu za Makonde katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji mnamo mwaka 1952
huku Jina la ugonjwa likiwa na asili ya Kimakonde lenye maana ya
“kilichopinda” yaani hali ya kupinda mwili inayotokana na maumivu makali
ya viungo kunakosababishwa na ugonjwa huu.
Kwa
upande mwingine Mhe. Ummy alithibitisha juu ya kuwepo kwa ugonjwa wa
Dengue nchini hususani katika jiji la Dar es salaam huku idadi ya
wagonjwa ambao wamethibishwa kwa kipindi cha Januari hadi Mei ni 226
ambao wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam.
‘Dengue
ulithibitishwa kuwepo hapa nchini hususani jijini Dar es Salaam kuanzia
mwishoni mwa mwezi wa Januari 2018. Hadi kufikia sasa idadi ya wagonjwa
ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huu kwa kipindi cha Januari hadi
Mei ni 226 ambao wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam. Vilevile
ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani umewahi kuripotiwa katika miaka ya
2010, 2013 na 2014” alisema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy ameeleza dalili za ugonjwa wa Dengue zinashabihiana amabazo
ni pamoja na homa ya ghafla, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na
uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza siku ya 3 hadi 14 tangu mtu
alipoambukizwa virusi vya magonjwa haya. Wakati mwingine dalili za
magonjwa haya yanaweza kufanana sana na dalili za ugonjwa wa malaria.
Vilele mara nyingine magonjwa haya yanaambatana na kutokwa na damu
sehemu za fizi, mdomoni, puani, kwenye macho na pia kwenye njia ya haja
kubwa au ndogo.
Kwa
upande mwingine Waziri Ummy amethibitisha kuwa hadi sasa nchini
Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na
virusi vya Ebola, huku kwa tathmini ilifanyika na Shirika la Afya
Duniani (Regional Risk Assessment) imesema kuwa Tanzania ipo kwenye
uwezekano wa kupata ugonjwa wa Ebola na imewekwa katika kundi la pili
miongoni mwa nchi 6 zilizo katika hatari ya kupata maambukizi zaidi,
kutokana na kupakana na nchi ya DRC pamoja na mwingiliano mkubwa wa watu
wake.
Pia
Mhe. Waziri amewatoa hofu Wananchi na kuwataka kuendelea kuchukua
tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu
aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchini, huku akiwaonya
wanaosambaza taarifa za uzushi juu ya uwepo wa ugonjwa huu na kuwataka
waache haraka.
Aidha,
Wizara itaendelea kushirikiana na Sekta mbalimbali katika kuimarisha
ufuatiliaji na kuendelea kutekeleza mikakati ya kudhibiti ili ugonjwa
huu usiingie nchini na kuendelea kutoa taarifa pamoja na Elimu kwa Jamii
kadri itakavyohitajika.

No comments:
Post a Comment