Wednesday, August 22, 2018

IBUNGILO YAICHAPA NYAMANORO ANGELINE JIMBO CUP 2018

Timu ya Kata ya Ibungilo imeendelea na ubabe wake kwa kuifunga Timu ya Kata ya Nyamanoro magoli manne kwa sifuri ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya mpira wa miguu ya Angeline Jimbo Cup 2018 yaliyobebwa na kauli mbiu ya ‘MICHEZO NI AJIRA’ mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kona ya Bwiru wilayani Ilemela. 

Katika Mchezo huo, Goli la kwanza la Timu ya Ibungilo lilifungwa na mchezaji Said Said dakika ya 18 kipindi cha kwanza,  Kisha mchezaji Didas Msafiri kuiongeza goli la pili dakika ya 19 kufuatia makosa ya kiufundi yaliyofanywa na mabeki wa Timu ya Kata ya Nyamanoro, Katika kipindi cha pili mchezaji Saidi Said akaiongezea tena Timu yake ya Ibungilo magoli mawili dakika ya 48 na dakika ya 61 hivyo kuifanya Timu yake hiyo kuwa na jumla ya magoli manne kwa sifuri hivyo kufuzu kuingia hatua ya Robo fainali ya mashindano hayo. 

Wakati huo huo, Katika kiwanja cha Sabasaba Timu ya Kata ya Kiseke imechuana vikali na Timu ya Kata ya Nyasaka mchezo ulioisha kwa sare ya  kufungana goli moja kwa moja, Goli la Timu ya Kata ya Nyasaka likifungwa dakika ya 3 na mchezaji Baraka Baraka kabla mchezaji Musa Shaban wa Timu ya Kiseke kusawazisha dakika ya 80 ya kipindi cha pili, Akizungumza mara baada ya kuisha kwa mchezo huo Kocha wa Timu ya Kata ya Nyasaka Ndugu Martine Jovine amewaasa mashabiki wa Timu yake kuendelea kuiunga mkono Timu yao ili izidi kufanya vizuri katika mechi zinazofuata huku Kocha wa Timu ya Kiseke Ndugu Victor  Enock akilalamikia waamuzi wa mchezo huo akidai wanaihujumu Timu yake kwa kuandaa matokeo kabla ya kuanza kwa mchezo.

Katika Uwanja wa shule ya msingi Buswelu, Timu ya Kata ya Mecco imekutana na Timu ya Kata ya Kahama, Mchezo ulioisha kwa Timu ya kata ya Mecco  kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli mbili kwa moja, magoli yaliyofungwa na mchezaji Silvester Godfrey dakika  ya pili, na dakika 78 mchezaji Paul Scholes kuiongezea goli la pili huku Timu ya Kata ya Kahama ikiambulia goli moja kutoka kwa mchezaji Regan John dakika ya 66.

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’








No comments:

Post a Comment