Friday, August 24, 2018

POLE..! POLE..! POLE..!

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula anatoa pole kwa Wananchi, Wazazi, Walezi na Uongozi wa Shule ya Nyamuge iliyopo Kata ya Nyasaka wilayani Ilemela kufuatia ajali iliyohusisha gari la Shule hiyo na kusababisha majeruhi na kifo cha dereva wa gari hilo.

Aidha anawaasa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria pindi wanapoendesha vyombo vya moto barabarani pamoja na kuwaombea wanafunzi wote waliojeruhiwa wapone haraka ili waweze kuendelea na masomo yao.

' Mkono wa uponyaji wa Mungu usiwapungukie, Na wapone haraka ameen '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela.
24.08.2018.




No comments:

Post a Comment