Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mhe Anthony Mavunde amefunga Semina ya Ujasiriamali leo tarehe
19/9/2018 ambayo imeendeshwa kwa muda wa siku tatu tangu Tarehe 17/9/2018.
Kabla hajafunga mafunzo hayo Mgeni Rasmi Mh Anthony Mavunde Amempongeza
M/Kiti wa UVCCM Mkoa wa MwanzaMh.Jonas Lufungulo na kamati yake nzima kwa kuandaa Semina hii
kwani itasaidia kuwainua vijana kimaendeleo na kiuchumi.
Mgeni Rasmi Mh. Anthony Mavunde amewaasa Vijana wote waliohudhuria
mafunzo hayo kwa siku tatu kuhakikisha wanayafanyia kazi yote waliyojifunza kwa
vitendo. Aidha amemshukuru Mkufunzi ndugu Kenani
Kihongosi ambaye pia ni M/Kiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa kwa kujitolea kutoa
mafunzo hayo kwa mda wa siku tatu na pia amemuahidi kuwa ipo siku atamuita
kwenye jimbo lake ili atoe simina hii kwa kata zote.
Mh Anthony Mavunde amesema
mambo mengi ya muhimu mojawapo
“Natamani kuwaona
Vijana wa Mkoa wa Mwanza, Mkoa wenye rasilimali za kutosha uwe mfano wa kutosha kwa vijana wa mikoa
mingine kwamba mnauwezo wa kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi.”
Pia
“Sisi
na Ofisi ya Waziri Mkuu tumeandaa muongozo
ambao kijana ambaye amemaliza
chuo kikuu ukileta maombi ofisini kwetu
tunakusaidia kukutafutia
makampuni mbalimbali kutokana na fani uliyosomea, anakwenda kujifunza kwa miezi 6 hadi 12 na badae atapewa cheti cha kumtambua
hata akienda kuomba kazi kampuni
nyingne inakuwa rahisi kupata”
Aidha
Mh Anthony Mavunde Amegawa Vyeti kwa kila wilaya ambazo zimehudhuria siku zote
tatu.
Imetolea
na




No comments:
Post a Comment