Umoja
wa Vijana CCm Mkoa wa Mwanza Umeandaa kongamano kubwa la Ujasiriamali litakalo fanyika kwa siku tatu(3) kuanzia tarehe 17 – 19/09/2018.
Akizungumza
M/kiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza ndugu Jonas Rufungulo ameelezea namna ambavyo kongamano litakavyo
kuwa la aina yake. Ameeleza mambo ambayo vijana na wasio vijana watakavyonufaika na semina hii kubwa ya
Ujasiriamali, Moja ya mambo aliyoyaeleza ni pamoja na watu kujifunza mambo
mengi kama vile kutengeneza batiki, vikoi pamoja na ufungaji.
M/kiti
wa UVCCM mkoa wa Mwanza ameeleza kuwa mgeni rasmi wa kufungua semina hii ni
M/kiti wa UVCCM Taifa Mh. Kheri Denis
James na Tarehe 19/09/2018 ambapo
itakuwa mwisho wa semina hii itafungwa na Mh Anthony Mavunde ambaye ni Naibu waziri Vijana ajira
na kazi.
Aidha
M/kiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza
amesisitiza watu waote kufika katika semina hii bila kuangalia chama, dini
kabila na hata rangi, hii ni semina ya watu wote wakubwa kwa wadogo na hakuna
kiingilio amesisitiza zaidi.
Aidha hadi sasa watu mbali mbali wameshaanza kujitokeza pamoja na viongozi mbali mbali wa UVCCM idara mbalimbali hapa jijini Mwanza miongoni ni Katibu wa UVCCM Mwanza Ndugu Odilia Batyomayo, M/kiti Mkoa Seneti Mkoa wa Mwanza Bi. Lwiza Mwenda, Katibu wa Wilaya ya Ilemela Mh. Nehemia Philimon na Wengine weng.
Karibuni
sana tujifunze Elimu ya Ujasiriamali.
Imetolewa
na
Ofisi ya
Katibu UVCCM Mkoa wa Mwanza

No comments:
Post a Comment