Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema Tanzania haina
mgogoro wa kibiashara na Kenya licha ya nchi hizo mbili kupitia mamlaka
zake kuzuia bidhaa mbalimbali zinazoingizwa kwenye nchi hizo.
Septemba
13 na 15 mwaka huu kulisambaa taarifa kuwa mamlaka ya mapato ya Kenya
KRA ilizuia malori ya mchele yaliyotoka Tanzania kwa madai ya mchele huo
kutokua na viwango vya ubora vilivyowekwa na nchi hiyo.
November
2017 kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliviteketeza kwa moto
vifaranga vya kuku 6,400 na Februari 2018 viliteketezwa vifaranga 5000
kwa kuingizwa bila kufata taratibu na sheria za nchi.
Akizungumza
na kituo cha EATV, Charles Mwijage amesema serikali ya Kenya na
Tanzania hazina mgogoro wa kibiashara bali kinachofanyika ni usimamiaji
wa taratibu zilizowekwa na mamlaka za nchi hizo huku akiahidi
kulifatilia suala la malori ya mchele ya Tanzania yaliyozuiliwa Kenya.
“Nimelisikia
hilo suala la kuzuiwa kwa malori ya mchele ya Tanzania, kimsingi hatuna
mgogoro wa kibiashara kati yetu na jirani zetu (Kenya) bali
ninachowaasa wafanyabiashara wetu wazalishe vitu vyenye ubora unaoendana
na viwango vya mataifa wanayopeleka bidhaa zao.”
Februari
mwaka huu nchini Uganda Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta waliwaagiza mawaziri wa pande zote mbili
zote kukutana kabla matatizo yanayojitokeza hayajifika kwenye ngazi yao.

No comments:
Post a Comment