Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula anawatakia kheri wanafunzi wote wa Kidato cha nne wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Siku ya leo Jumatatu Novemba 05, 2018.
Aidha anawaasa wahitimu hao kuwa waadilifu na kuzingatia taratibu zote za mitihani kwa kujiepusha na udanganyifu ili kupata wahitimu wenye weredi wa hali ya juu na wataalamu wa baadae au viongozi ambao hawatatiliwa shaka.
Zaidi ya watahiniwa 427,000.00 wanatarajiwa kufanya mtihani huo kwa nchi nzima, Wakati Jimbo la Ilemela wakifanya watahiniwa 6,253 wavulana wakiwa 3,111.00 na wasichana wakiwa 3,142.00 kutoka Shule 23 za Serikali na 20 za binafsi na kituo kimoja cha mtihani.
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
05.11.2018.


No comments:
Post a Comment