Saturday, November 10, 2018

KONGAMANO LA VYUO NA VYUO VIKUU LAFANYIKA LEO

Leo linafanyika Kongamano la Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Mwanza ambapo watoa mada mbali mbali wameendelea kutoa Darasa la Uongozi, Itikadi na Uenezi. Moja ya watoa mada ni Chief Missaga Mwenyekiti wa First Community, Devis Peter, Madam Lwiza na  Samson Chacha 

Aidha watoa Mada wanaelezea maana ya Uongozi, Uenezi na Uitikadi kwa kutoa mifano halisi ya utendaji Bora wa Serikali Yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Moja ya mambo yanayosisitizwa ni pamoja na kutoa sifa za kiongozi bora ambazo Kiongozi lazima ajiandae na matukio ya dharura kama vile mafuriko awe na nidhamu kazini pia Wajibu wa kiongozi katika jamii nikuhakikisha Elimu inapatikana.

Pia watoa mada wote wamewaasa wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii na huku wakiwa na malengo kwani baada ya masomo kuna watu wataajiriwa na wengine watajiari.

No comments:

Post a Comment