Gavana wa wilaya ya Ilemelea Ndugu Godfrey Mzava amewasisitiza wananchi wa wilaya hiyo juu ya umuhimu wa kuwa na ulinzi shirikishi utakaosaidia kupambana na kupunguza vitendo vya kiharifu hasa vile vya ukabaji na unyang’anyi.
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kiseke ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo hasa ujenzi wa madarasa na miundombinu ya afya, kutoa elimu juu ya katazo la matumizi, usambazaji na uzalishaji wa mifuko ya plastiki ambapo amewataka wananchi hao kuhakikisha wanakuwa na vikundi vya ulinzi shiriki ili kupambana na vitendo vya kiharifu vinavyoendelea katika kata hiyo baada ya kutokea matukio kadhaa ya ukabaji na uporaji mida ya usiku
‘.. Niwaombe kuhakikisha tunaanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na vitendo hivi vya kiharifu vinavyoendelea ndani ya kata yetu, Na hawa waharifuhawatoki mbali tuko nao kila siku katika maeneo yetu tuungane pamoja na vyombo vya usalama kuwadhibiti ..’ Alisema
Aidha Gavana Mzava ametumia mkutano huo na wananchi kuendesha zoezi la upigaji wa kura za Siri ili kuwafichua watu wanaodhaniwa kuwa ni waovu wanaotekeleza vitendo hivyo vya kiharifu na baadae kumkabidhi polisi wa kata ya Kiseke maajina hayo kwaajili ya upelelezi zaidi huku akiwahakikishia wananchi hao kuwa yeyote atakaebainika kuhusika na matukio hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Kiseke, Kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo, Amemshukuru Gavana Mzava kwa ziara yake yenye tija kwa wananchi anaowahudumia huku akibainisha shughuli za maendeleo zinazoendelea ndani ya kata yake, Pamoja na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa na ofisi yake katika kupambana na vitendo vya kiharifu kwa ngazi ya kata huku akiahidi kulifanyia kazi wazo la kuhamasisha wananchi juu ya kuwa na vikundi vya ulinzi shiriki katika maeneo yao ili kupambana na kadhia hiyo.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’





No comments:
Post a Comment