Sunday, July 7, 2019

BARAZA LA UVCCM MKOA WA MWANZA LAMPONGEZA MHE RAIS JPM KWA KAZI NZURI ILIYOTUKUKA YA KULETA MAENDELEO MAKUBWA KWA KIPINDI KIFUPI KWA WATANZANIA

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm mkoa wa mwanza comrade Jonas Lufungulo  amempongeza  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe  John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo WATANZANIA kwa kipindi kifupi alicho kaa madarakani_matokeo chanya yanaonekana katika sekta zote mfano
Afya,Elimu,miundo mbinu,usafiri wa anga ,*NK

Katibu wa umoja wa vijana mkoa wa mwanza comrade Dennis Luhende   alitumia kikao hicho cha baraza kuwaasa vijana kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kuwa watiifu juu ya maagizo na maelekezo yanayo tolewa na viongozi wa ngazi za juu

Mbunge wa viti maalumu kupitia vijana
bi Maria Kangoe  akiongea na wajumbe wa baraza la vijana mkoa wa mwanza aliwapongeza wajumbe wa baraza kwa kuwa wabunifu wa kuanzisha miradi ya kiuchumi

Bi Maria Kangoe ameamuwa kuwaunga mkono vijana kwa kuwapatia nyenzo za mashine za kufanyia kazi ilikuendana na Tanzania ya viwanda

kupitia baraza hilo mbunge wa vijana alikabidhi mashine ya  kuchomelea kwa vijana wa wilaya ya misungwi ikiwa ni mwendelezo wake wakutoa nyezo kwa vijana wilaya zote za mkoa wa mwanza

Pia kikao hicho kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa vijana Taifa (MCC) Comrade KherMwenyekiti ambae ni mjumbe halali wa baraza la vijana mkoa wa mwanza kwa mujibu wa kanuni ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi

Mwenyekiti wa vijana Taifa aliwasii vijana kuendeleza misingi ya umoja ,mshikamano, upendo na uzalendo kwa lengo la ujenzi wa Taifa letu

Hussein  A Kimu
Katibu hamasa,chipkizi,Sera na utafiti uvccm mkoa wa mwanza

TUKUTANE KAZINI























No comments:

Post a Comment