Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula hivi Leo amefunga Mashindano ya kombe la Malando Ndondo wilayani Ilemela lililofadhiliwa na Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi na Mbunge Jimbo la Ilemela Dkt. Angelina Mabula na kuvikutanisha vikosi 16 dimbani kutoka Kata ya Bugogwa.
Mhe. Mabula akifunga michuano hiyo, amempongeza Mhe. Angelina Mabula kwa kazi kubwa anayoifanya kuibua, kuinua na kuendeleza michezo kwa wana Ilemela na kuwaomba wananchi wazidi kumpatia ushirikiano kwa mstakabali wa maendeleo ya Jimbo Lao. Kadharika Mhe. Mabula amekabidhi Ng'ombe watatu kikosi cha Simba S.C Igombe kwa kuibuka kidedea katika michuano hiyo dhidi ya kikosi cha Yona FC kilichoshika nafasi ya pili na kuambulia Ng'ombe wawili. Washindi wengine walipata zawadi ni pamoja na mshindi wa tatu ambaye alipata Ng'ombe mmoja, na Mchungaji bora na Mchezaji bora Tsh. 20,000 kwa kila mmoja.
Fainali hizo zimehudhuriwa na Ndg. Kazungu Katibu wa Mbunge Jimbo la Ilemela, Diwani mwenyeji Mhe
Mshamba, Mwenyekiti wa UVCCM Ilemela, Mratibu wa kombe la Marando Ndondo Ndg. Matthias, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Organisation Ndg. Ahmed Misanga pamoja na Afisa Tarafa Ilemela Ndg. Mzava.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana







No comments:
Post a Comment